Diamond Platnumz Atajwa Tuzo za MTV EMA
Staa Wa Muziki kutoka Africa Diamond Platnumz amechaguliwa kuwania Tuzo za MTV Europe Music Awards Mtvema 2024 katika kipengele cha msanii bora kutoka Afrika akichuana vikali na Asakemusic, Ayrastarr (Nigeria), Tyla , Titom & Yuppe, DBN Gogo (Afrika Kusini).
Diamond ameteuliwa kwa mara nyingine kwenye MTV EMAs mwaka huu, baada ya 2023 Kushinda, akiwa msanii pekee kutoka Afrika Mashariki Aliyekuwa Akiwania Tuzo Hizo Ambapo Alikuwa Akishindana Na Wakali Wengine Wa Nigeria Kama Vile Burna Boy, Asake N.k
Zoezi La upigaji kura umeanza rasmi kwenye website ya mtvema.com ambapo zinatarajiwa kufanyika Novemba 10, 2024 Huko Mjini Manchester Nchini Uingereza
Lakini Pia Diamond Ndio Msanii wa kwanza Afrika kushinda tuzo 3 za MTV European Music Awards (EMAs). Aliwahi kushinda tuzo mbili (2) ya BEST AFRICAN ACT na BEST WORLDWIDE ACT (AFRICA/INDIA) ndani ya usiku mmoja mwaka kwenye 2015 MTV EMAs Na Nyingine Ya ‘Best African Act’ Mwaka Jana 2023
Etiket
new
trending
Subscribe Our Newsletter
0 Comment
Post a Comment
Your thoughts and opinions matter. Leave a comment below DO NOT SPAM!